Jumatatu, 11 Februari 2013


BW.ATHUMANI HUSSEIN HUSSEIN SESEME
je, unafahamu kuwa mzee Athumani ndio mtotot wa kwanza kati ya watoto 16 wa mzee seseme makumbitu?
 fuatilia kwa makini historia yake.

Inakubalika kwamba safari yoyote ile haikosi kiongozi wake. Na katika uzawa wa ukoo huu wa Seseme hapana shaka kiongozi wake ni Bw ATHUMANI                Hussein mtoto wa kwanza wa Mzee Hussein Hussein Seseme. Umefikiwa uwamuzi wa kumtambua hivyo mzee Athumani kuwa huyo ndiye kiongozi wa ukoo huo wa          Seseme kutokana na yeye mwenyewe kufanya mambo mengi mazuri katika kusaidia ukoo kuimarika japokuwa mzee Athumani alikuwa mtoto wa tatu kiuzawa  kuzaliwa. Baada ya kuanza kuzaliwa Bi Mwanakheri Omari Seseme, akifuatiwa na Bi Amina Abdallah Seseme ndipo kisha  akazaliwa yeye bado fikra za wengi zilimpa nafasi kubwa ya uongozi Mzee Athumani. Ni mambo mengi mazuri alioyafanya katika ukoo huu ambayo yangefaa kupigiwa mfano lakini tunachelea kuandika hapa kila jambo kwani itakuwa ni hadithi ndefu kama vile alifu lela ulela. Kwa kifupi mzee Athumani alizaliwa mwaka 1922 bila shaka hapo Mtoni kwa Azizi Ally, na alifariki nyumbani kwake Bungoni Ilala Dar es salaam mnamo tarehe 29/9/2008.

 Mzee Athumani walizaliwa wawili tu upande wa mama yake Bi Chausiku Binti Mwenegoha Kawambwa wa Kingugi, katika ukoo wa Dumbalume. Bi Chausiku alikuwa mke wa kwanza kuzaa na mzee Hussein Hussein.   Maisha ya bibi huyo yaliishia Mtoni kwa Azizi Ally   baada ya kwisha kuzaa wanawe wawili hao, mzee Athumani Hussein na dada yake Bi Mwajuma Hussein, Bi Chausiku                            alipofariki miaka ya 19 hivi alizikwa pembezoni mwa msikiti wa kwa Kombo hapo hapo Mtoni. Aliwaacha Mzee Athumani na dada yake Bi Mwajuma wakiwa bado wadogo sana.

ELIMU.
Mzee Athumani Hussein alipata elimu zote mbili ya dini na dunia , hivyo katika elimu ya dini ya Kiislamu imemjengea imani kubwa katika Uislamu hadi kuwa muumini wa kweli wa Kiislamu ambaye akifuata  maagizo yote ya dini itikadi.              Alikuwa Hamsa swalawat asiyependa kupitwa na hata kipindi kimoja cha swala katika umri wake wote hadi alipofariki.


Kwenye miaka ya hamsini hadi sitini alipata kuwa Imamu wa msikiti wa Keko Akida katika kipindi Fulani,, alipokuwa akiishi hapo kati ya mwaka 1952 hadi 1963 mzee Athumani alihamia Keko Akida katika mwka 1952 akitokea Mbagala, kabla ya hapo alipata kuishi mtaa wa Nyamwezi na Kipata eneo la Kariakoo mahala    ambapo mtoto wake wa kwanza Bw. Hassan    Athumani Seseme alipozaliwa kwenye miaka ya 1946 kabla ya kuhama tena na kurudi Mbagala kipindi chote hiki                 alishaanza kufanya kazi Railways  alipoanza kazi Railwaya kunako mwaka 1940 akiwa na umri wa mika 19 hivi.

Akiwa kazini Railways alipata kupelekwa masomoni Nairobi Kenya katika               kuboresha ujuzi wake kama Locomotive Mechanic katika idara ya fittingi shop. Na aliporudi masomoni akapata cheo cha foreman na hatimaye Supervisor. Cheo hiki alidumu nacho hadi pale alipostaafu rasmi mwaka 1977.

Alipohamia Ilala Bukoba Street 31 mwaka 1963 mwishoni aliendelea na Uimamu, hapo alisalisha msikiti wa Pangani na Mwanza mara baada ya kufariki Imamu wa msikiti huo kwenye miaka ya sabini themanini hivi.

Vile vile aliendelea na Uimamu katika msikiti mkuu wa Ilala, Arusha Street kwa muda fulani mwisho alimalizia uimamu katika msikiti wa masjid Taqwa Bungoni wakati huo alikuwa hajiwezi tena kwa kuzidiwa na umri na maradhi ya kiutu uzima.
 Mzee Athumani katika ujana wake wote na hata alipofika kuwa mtu mzima alijishughulisha mno na  mambo ya dini ya Kiislam. Alipenda kujiendeleza kusoma dini na pia alikuwa mwana Twarika mashuhuri sana wa “SHADHIRY”.
Miaka ya 1977 alipostaafu kazi Railways alipata bahati ya kwenda HIJJAH MAKKA.  Kutokana na kujishughulisha sana na mambo ya dini alipostaafu kazi alifanya kazi ya dini BAKWATA, kutokana na uadilifu aliwahi kuchaguliwa na BAKWATA kuwa Sheikh wa Wilaya ya Ilala cheo hicho alidumu nacho hadi kifo chake mnamo mwaka 2008.
Bwana Athumani katika elimu ya dunia alipata kusoma shule ya Mchikichini na hatimaye akaendelea na masomo yake katika shule ya Uhuru Mchanganyiko enzi hizo ikijulikana kama Kitchwele Boys Middle School. Hapa alisoma hadi darasa la nane kisha kujiunga na Railwaays 1940 . Kichwele Boys alipata kusoma na baadhi ya viongozi wa nchi hii Tanzania kama vile mzee Kawawa, Kitwana Kondo na kadhalika . Aliwahi pia kuwa kaka wa shule Prefect hapo Kichwele School.

Inasemekana kuwa elimu yake ya dini alisoma katika madrasa ya maalimu Mzinga eneo la Kariakoo lakini kwa vyovyote vile enzi hizo Masheikh                    waliokuwa wakifundisha walikuwa siyo hawa kina maalim Mzinga                           tunayemfahamu sisi. Kwani kipindi hicho tunachokiongelea ilikuwa miaka ya 1930/1940. Ni yule maalim Mzinga mwenyewe hapo awali aliwahi kusoma             Madrasa  ya baba yake Mzee Makumbitu hapo Mtoni.

Bw. Athumani aliwahi kuoa jumla ya wake wanne wakati wa uhai wake, kila mke kwa wakati wake, hakuwahi kuwa na mke japo wawili tu kwa wakati mmoja.
Mke wa kwanza wa mzee Athumani aliitwa Tuhuma bint Omari alimuoa mwaka 1940. Aliishi naye kwa takribani miaka mitano hivi, lakini Bibi huyu hakuzaa, alikuwa hana kizazi, mnamo mwaka 1945 alimuoa Bi Mwanaasha binti              Mwinyihija Minjuma Kuchimba kutoka Mtoni Kijichi baada ya kumuacha          Bi  Tuhuma.Bi mwanaasha alizaliwa mwaka 1930 alipofunga ndoa alikuwa na umri wa miaka 16 tu.

Mzee Athumani alizaa watoto kumi  na mbili (12) na Bi Mwanaasha mnamo mwaka 1969 Mzee Athumani alimwacha Bi mwanaasha na akaolewa na mume mwingine ambaye alizaa naye watoto wawili (2) Bi Mwanaasha baadaye aliugua na kufariki nyumbani kwao Mtoni Kijichi. Mnamo August 1981. Aliishi na mzee Athumani kwa miaka takribani 36 (1945- 1981)

Mwaka 1971 Mzee Athumani alimuoa Bi Meje kutoka Buyuni waliishi miaka ishirini na saba (27) alifariki, Bi Meje hakuwahi kuzaa na mzee Athumani. Mwaka 2000 Mzee Athumani alimuoa Bi Nyapilimo Akaishi naye miaka mitano kisha mnamo mwaka 2005 akamuacha.  Baada ya hapo Mzee Athumani aliendelea kukaa bila ya mke hadi pale alipofariki 29/09/2008.  Bi Nyapilimo alifariki mwanzoni mwa 2012.
 Mzee Athumani hadi anafariki aliacha watoto wake walio hai wakiwa tisa ( 9) sita wanaume na watatu wanawake  Hata hivyo baada ya muda si mrefu watoto wake wawili walifariki, kwanza Bi Jamila Athumani aliyefariki tarehe07/02/2009   na baadaye Bw Talib Athumani aliyefariki tarehe 05/07/2009  miezi mitano          baadaye huko Boswana Gaberone na kuzikwa Mbagala Kizuiani maskani ya ukoo wa Seseme.   Watoto wengine wa mzee Athumani waliofariki huko nyuma ni kama ifuatavyo:
1. Hussein athumani                  amezaliwa  1948   amefariki 1949
2. Chausiku Athumani amezaliwa 1950 amefariki  1952
Hadji Athumani amezaliwa  1956 amefariki  1997

Hadi sasa watoto walio hai ni saba (7) wakiwemo wanaume watano (5) na wanawake wawili (2) Watoto hao wanaume ni Hassan, Salama (Bapoo),            Muharami, Omari na Ishaka wanawake ni Subira na Salima.

Mzee Athumani Hussein ni mmoja wapo kati ya mifano bora kwa binadamu kuiga kwani siyo siri yeye amefanya mengi mno katika uhai wake kwenye ukoo ambayo wengi wetu hatujayafikia mambo hayo. Mzee Athumani hakua mbaguzi katika ndugu zake na hata wasio kuwa ndugu zake.

Mzee Athumani tokea miaka ile ya 1950 wakati wazee wetu watatu wote wako hai akina mzee Hussein Hussein, Omari Hussein na Abdallah Hussein                       wameshampa fursa ya kuongoza ukoo.

Naye akakipokea cheo hicho kwa roho moja na kukitendea haki. Hii ni            kutokana na tabia yake ya uadilifu.Dhamira ya mzee Athumani kwa ndugu zake ilikuwa ni kuwafikisha mbali kimaisha.

Na katika kuonesha jinsi alivyodhamiria kuwapeleka mbele kimaendeleo ndugu zake hao, wengi kati yetu alitulea kwa kutusomesha na kuhakikisha tunakuwa na maisha bora hapo baadaye,licha ya kuwalea wanawe wa kuzaa mwenyewe kama ilivyo wajibu lakini pia Bwana Jaffar Hussein Seseme, Mwishehe, Ashura, Ally na Husna ni kati ya wanandugu ukoo wa Seseme aliowahi kuwalea. Bwana Azizi  Kuchimba, Bi Zena Kuchimba nao ni miongoni mwa hao aliowahi kuwalea.  Hawa wakitokea upande wa mkewe. Pamoja na hao kuna wengine wengi aliopata kuwalea waliotokea aidha upande weke ama kwa mkewe, wote hawa aliwaona ni sawa hakujua kubagua.

Watu walimsifu kwa uungwana wake wamesema kuwa Mzee Athumani                    alikuwa ni muhimili mkubwa katika ukoo wa Seseme kwani hakujua kubagua yoyote wote kwake yeye walikuwa sawasawa mbele yake. Kwa kifupi cha             maneno Mzee Athumani alifananishwa na Jemedari shupavu, Amiri, Khalifa na Imamu katika ukoo wa Seseme.

Bwana Athumani wakati wa mazishi yake pale Mbagala Kizuiani watu wengi mbalimbali walihudhuria, wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume. Hiki                 kilikuwa kielelezo tosha cha umaarufu wake.