Jumamosi, 22 Juni 2013

NI MIMI NDUGU YENU BW SHABANI ALLY SESEME NAWALETEA MADA HII YA UMUHIMU WA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA UISLAMU BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIIM Assalam alaykum!! Utangulizi Kila sifa njema anastahiki kushukuriwa Allah(s.w),Rehma na amani zimuendee kiongozi wa ummah huu Mtume Muhammad(s.a.w) na juu ya aali zake na maswahaba zake wote(r.a Napenda kuchukua fursa hii tukufu ili niweze kuufikisha ujumbe huu kwa waislam juu ya Umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano baina yetu.Suala la umoja na mshikamano baina ya waislamu ni jambo ambalo Allah( s.w) analisisitiza sana katika kitabu chake kitakatifu.Hivyo basi umoja baina ya waislamu ni jambo la LAZIMA.Ukiangalia katika ibada zote alizotuwekea Allah(s.w) zinahimiza suala la kuwa na umoja na mshikamano baina yetu waislamu.Angalia tu katika nguzo za uislamu jinsi Allah alivyoziweka na zinavyohimiza umoja baina yetu ni wazi kuwa suala la umoja na mshkamano ni muhimu sana katika uislamu.Ibada ya Swala, Funga , Zakat, Hijjah n.k, hizi zote zina himiza umoja na mshikamano baina yetu. Katika kusisitiz suala hilo Allah anasema katika sura ya 49:10 “Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe. “ Katika aya hii tunajifunza kuwa waislamu wote ni nduga, pale linapotokea tatizo basi hapana budi watu wapatane ili tuweze kujenga umoja utakao kuwa madhubuti baina yetu.Lakin leo ni tofauti waislam wao kwa wao ndio hugombana, hitiliana fitna, majungu n.k hii ni kuonyesha leo hakuna umoja na mshikamano uliopo baina yetu. Kaika maubile ya wanaadamu suala la ikhtilafu ni la kawaida.Allah ametuumba tofauti tfauti wapo wanene, wembamba,warefu, wafupi, weupe, weusi , hizi ni tofauti.Kuzuia ikhitilafu hutoweza kwa sababu ndio maumbile ya mwanaadamu,asichotaka Allah ni FARQA. FARQA baina ya waislam in jambo ambalo Allah alikemea na halipendi anachotaka yeye ni umoja (I’TISWAM) na mshikamano baina yetu.Anasema katika Qur-an sura 3:103-105 “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka”.Anaendela nakusema .”Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa”.Anaendelea nakusema .”Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa. “. Hizi ni aya ambazo Allah anasisitiza waislam tuwe na umoja na mshikano na yeye hapendi kufarikiana katika masiala ya dini na ndio maana yeye anatuambia pale tunapo ikhtilafiana katika masuala ya dini tufanye yafuatayo.Qur-qn 4:59 ‘Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” Hivi ndivyo Allah anavyo tufundisha tufanye pale tu tunapo ikhtalifiana katika masuala ya dini yetu nayo ni kuirejea QUR-AN na SUNNAH hiyo ndiyo suluhisho litakalopelkea kupatana kwetu.Sasa basi kwa nini mpaka leo waislamu wamefarakana?.Jibu ni kwamba waislamu tumeacha kuifuata QUR-AN na SUNNAH na ndio maana leo tupo kwenye hali hii. Hivyo basi Allah anatutaka tuifuate QUR-AN na SUNNAH kwani ndio vitu viakavyo tuletea umoja wa kweli na mshikamano baina yetu waislamu.Allah katika Qur-an anatuelelea kwamba yeye anawapenda watu walioshikamana katika dini yake.Anasema katika sura ya 61:4 “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana” Allah anaupigia mfano umoja na JENGO jinsi (material) yaliyo tumika kulitengeneza jingo yalivyo shikamana,.Kama hivyo ndivyo mtume (s.w) anasisitiza katika hadithi ifuatayo: Imepokelewa hadithi kutoka kwa Nu’uman bin Bashiir (r.a).Mtume anasema”Waumini ni sawa kama macho yanauma (yana matatizo)mwili mzima unaumwa (una matatizo) kama kichwa chake kinauma basi wmili mzima unauma”(Muslim) Ndugu zangu katika imani hivi bado hujaelewa tu jinsi suala la umoja na umoja na mshikamano lilivyo kuwa muhimu katika uislamu. Mafunzo tunayoyapata kutokana na aya hizi na hadithi hii ya mtume(s.w) 1. Umoja ni jambo la lazima 2. Atakaye vunja umoja amekeuka amri ya Allah 3. Kpendana baina yetu 4. Umoja na mshikmano ndio ngao kwa waislam. Allah anatukataza katika Qur-an kuwa na makundi makundi makundi katika dini yetu kwani kila kikundi kitasifia upande wake na FARQA itatokea.Allah ansema katika sura ya 30:31-33 “ Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Sala, na wala msiwe katika washirikina”.Anaendelea “. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho”Anaendelea “ Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi,” Ili tuwe na umoja na mshikano kama alivyokuwa mtume na maswahaba zake uliopelekea kuwashinda maadui wa zama zao, Allan anasema sura ya 48:29 “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.’ ni lazima umoja huo upitie upitie hatua TATU: 1. Tuwe na lengo moja.(9:33, 61:9, 48:28) 2. Kufanyiana wema baina yetu(hadithi ya mtume) 3. Kutofanyiana mabaya · Dhulma · Kusengenyana · Kuchukiana · Kuvunjiana heshma Sababu za kutokuwa na umoja na mshikamano 1. Hatuna lengo moja 2. Ufahamu wetu juu ya dini tofauti 3. Ufahamu wetu juu ya qQur-an ni tafauti 4. Ufahamu wetu juu ya sunnah ni tofauti Hitimisho:Hivyo basi waislamu ni lazima tushkamane na tuwe na umoja wa kweli baina yetu ili tuzishinde kaumu za makafiri